System Logo

Okoa ni mfumo wa kompyuta unaotumiwa kwa pamoja na wadau wote wa afya ambao ni Vituo vya Afya, Bohari (Stoo) Za Madawa Za Serikali (MSD),Wizara Ya Afya, Halmashauri na Wananchi huku kila mmoja akiweza kupata taarifa zinazomuhusu tu. Mfumo huu unawezesha kudhibiti wizi wa dawa katika Vituo vya Afya vya Umma ili kuwahakikishia wananchi kupata dawa za bei nafuu zilizonunuliwa kwa kodi zao wenyewe na hivyo kuwapunguzia gharama za matibabu, kuwaokolea maisha, kuwaokolea muda na kuwaokolea muda wa kukaa kwenye foleni wakisubiria huduma, na kuokoa pesa zetu za kodi zinazotumika kununua dawa huku baadhi ya dawa zikiishia kuibiwa na wafanyakazi wachache kwa maslahi yao binafsi

Okoa itamsaidia mwananchi kujua vituo ambavyo dawa zipo katika eneo lake ili aende akiwa na uhakika wa kupata dawa na pia itamjulisha mwananchi hali ya foleni katika vituo vya afya katika eneo lake ili aweze kwenda sehemu yenye foleni ndogo lakini yenye dawa.

Okoa imetengenezwa na Mr. Bukhary Kibonajoro na inamilikiwa na Kampuni aliyoianzisha mwaka 2015 iitwayo StraightBook Limited yenye makao makuu Dar es salaam na ofisi ndogo Kigoma.
Mr. Bukhary Kibonajoro alichaguliwa mwaka 2015 miongoni mwa wahandisi wabunifu (Engineering Innovators) 12 bora barani Afrika na Taasisi kubwa kabisa ya maswala ya Uhandisi (Engineering) ya nchini Uingereza iitwayo Royal Academy Of Engineering kwa ajili ya kushindania Tuzo kubwa kabisa ya maswala ya Uhandisi barani Afrika iitwayo Africa Prize for Engineering Innovation kwa ajili ya yeye alivyotengeneza mfumo huu wa Okoa.
Pia kwa kutengeneza mfumo huu wa Okoa, Mr. Bukhary Kibonajoro mwaka huu 2017 ameshinda shindano liitwalo Data For Local Impact Innovation Challenge linalodhaminiwa na Serikali ya Marekani kupitia taasisi iliyo chini ya Ofisi ya Rais wa Marekani ya PEPFAR(The United States President's Emergency Plan For Aids Relief) na kusimamiwa na MCC (Millenium Challenge Corporation) na shindano hilo linaendeshwa na taasisi ya Dar Teknohama Business Incubator iliyo Tume ya Taifa Ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia mpango mkubwa wa Data Collaboratives for Local Impact.

Okoa imefungwa na kutumika Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa udhamini wa Serikali ya Marekani kupitia PEPFAR mwaka 2017 na matumaini ni kusambaa halmashauri zote nchi nzima hivi karibuni ili kutatua changamoto katika sekta ya Afya nchini kwetu.